Saturday, August 7, 2010

WAJUMBE WA AALCO KATIKA DINNER

Waziri wa Katiba na Sheria na mtetezi wa kiti cha Nachingwea kule Lindi Mathias Chikawe a.k.a Matth akiongea katika 'Cocktail Party' iliyoandaliwa na Ubalozi wa Japan kwa wajumbe wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya Kisheria baina ya nchi za Asia na Afrika (AALCO). Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa na kulia ni Kiongozi wa Ujumbe wa Japan katika Mkutano huo Balozi Yasuji Ishigaki. Hii ilikuwa Kilimanjaro Kempinski Hoteli jana Ijumaa, Agosti 6. Wadau wa sheria katika hafla hiyo...kulia ni Anselem Mwampoma, Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka; kati ni brazameni Kamana Kamana, Wakili wa Serikali na kushoto ni Mathew Mwaimu, Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Washkaji wengine pia walikuwepo, kulia jamaa anaitwa Bujiku, yupo Foreign pale akiwa na mgeni wake.
Na wenyeji wengine pia walikuwepo...Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mashtaka Eliezer Mbuki Feleshi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Mkuu wa kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo Oliver Mhaiki, Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Rahmat Mohamad na Dkt. Gerald Ndika, Kaimu Mkuu wa Law School of Tanzania au kwa kibongo Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania.
Hapa Matth akipiga 'toast' na Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa (kati) na Kiongozi wa Ujumbe wa japan katika mkutano huo Balozi Yasuji Ishikagi katika halfa hiyo.
Waziri Chikawe akiongea na Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Rahmat Mohamad (kulia) na Kiongozi wa Ujumbe wa Sri Lanka katika mkutano huo Priyasath Gerard (kati) katika hafla hiyo.
Sikia kijana...Matth akimpa maneno Dkt. Gerald Ndika, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania maarufu Law School of Tanzania katika hafla hiyo. Kati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Oliver Mhaiki.
Mama mbele anapiga kiswahili safi...anaitwa Suad Mohamed Al-Lamki, Mshauri Mkuu wa masula ya sheria katika Wizara ya Sheria ya Oman. Mama aliwahi kukaa Bongo miaka ya 70 akipiga kazi. Mdada nyuma ni Sarah Hamad Al-Sharji na jamaa kulia ni Saif Nasser na mshkaji kati ni Ahmad Khalifa wote kutoka Oman wakiwa katika hafla hiyo.