Friday, December 3, 2010

Viongozi TLS wametembelea Waziri Kombani ofisini

Waziri wa Katiba na Sheria a.k.a WKS Celina Kombani akipokea taarifa mbalimbali za Chama cha Wanasheria nchini (TLS) kutoka kwa Rais wa Chama hicho Felix Kibodya leo. Rais huyo na baadhi ya wananchama wa TLS walitemtembelea Waziri huyo ofisini kwake.
Picha ya pamoja....
Mazungumzo kidogo...

Tuesday, November 30, 2010

UJENZI LAW SCHOOL WAANZA

Ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) utakaogharimu Tshs 16/- bilioni na kukamilika Februari 2012 umeanza katika eneo la ekari 23 lililopo mkabala na barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam. Ujenzi unagharamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Programu yake ya Maboresho ya Sekta ya Sheria. hafla ya kukabidhiwa eneo kwa kampuni ya Ujenzi ilifanyika hivi karibuni katika eneo hilo...
Bi. Anna Mayawalla aliyemwakilisha Katibu Mkuu akielekezwa kutia saini hati ya makabidhiano ya eneo. Wengine wanaotia saini ni Dkt. Gerald Ndika (kulia), Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo na Bw. Jia Jianhui, Meneja Mkuu wa Beijing Construction Group inayojenga majengo hayo.
Mchoro wa moja ya majengo ya Taasisi hiyo yanayojengwa mara likikamilika...
Bi. Anna Mayawalla akibadilishana hati walizotia saini na Bw. Jia Jianhui...
Mkurugenzi wa Co-Architecture Mhandisi Alloyce Mushi akiongea katika eneo hilo...

Kombani akutana na Watendaji Sheria

Waziri Mteule wa Katiba na Sheria Bi. Celina Kombani akiongea na Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake jana Makao Makuu ya Wizara hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu Bw. Oliver Mhaiki.
Msajili wa Mahakama ya Rufani Bw. Francis Mutungi akiongea katika mkutano na Mhe. Kombani jana jioni. Katikati ni Katibu Mkuu Bw. Oliver Mhaiki.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay akitoa brief kwa Waziri Mteule Bi. Kombani (hayupo pichani). Wengine kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Japhet Sagasii, Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Mathew Mwaimu, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Eliezer Feleshi, Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani Bw. Phocus Bampikya na Msajili wa Mahakama ya Rufani Bw. Francis Mutungi.

MAWAZIRI NA MANAIBU WAAPISHWA

Waziri mteule wa Katiba na Sheria akiapa mbele ya JK mwishoni mwa wiki Ikulu jijini Dar es Salaam...
Mhe. Clina Kombani akitia saini kiapo mbele ya JK...
Waziri mteule, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Matth Chikawe akiapa mbele ya JK kushika wadhifa wake mpya. Awali alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Bonge la kumbukumbu... Waziri mteule wa Katiba na Sheria Bi. Celina Kombani, Waziri akiyemkabidhi kijiti Bw. Matth Chikawe (shoto) na Katibu Mkuu Bw. Oliver Mhaiki viwanjani hapo...
JK akiwa na familia ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Matth Chikawe mara baada ya kumwapisha...
Waziri Mteule wa Katiba na Sheria Bi. Celina Kombani na Katibu Mkuu Bw. Oliver Mhaiki (kulia) katika picha ya kumbukumbu na wadau wengine wa sekta ya sheria na wanasiasa viwanjani hapo...
Mawaziri wateule Mustapha Mkullo (pili toka kushoto), Fedha na Uchumi na Matth Chikawe kulia wakiwa na familia na jamaa.
Baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara na Makao Makuu waliamua kupata picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo. Kutoka kushoto Mathew Mwaimu, Wanyenda Kutta, Casmir Kyuki, Eliezer Feleshi, Salome Mollel, Philip Saliboko na Christina Sonyi.
Mnyalu Hassan Mhelela wa BBC nae alikuwepo live...
Wanahabari nao pia walikuwepo kikazi...
Bi. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akiwa na ndugu na jamaa mara baada ya kuapishwa.

Monday, October 18, 2010

Wachina kujenga mejengo ya kudumu ya 'Law School' Sam Nujoma

Kulia Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Oliver Mhaiki na Meneja Mkuu wa Beijing Construction Engineering Group Company Ltd wakibadilishana mawazo kabla ya kutia saini mkataba wa ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania a.k.a Law School of Tanzania. Mkataba huo una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 16.
Kutoka kulia...Bw. Aloyse Mushi, Mtaalam Mshauri wa ujenzi katika ujenzi huo; Bw. Juvenalis Motete, Mratibu wa LSRP; Bw. Benas Mayogu, Afisa Ugavi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Dkt. Gerald Ndika wakiweka mambo sawa tayari kwa hafla ya utiaji saini...
Kulia (KM) Mhaiki na kushoto GM Jia Jianhui wakitia wino huku Bw. Benas Mayogu, Afisa Ugavi wa Wizara akicheck...
Kamata makabrasha haya...KM Mhaiki (kati) akimkabidhi Bw. Jia Jianhui 'dokumneti' zinazohusiana na ujenzi wa majengo ya 'Law School'. Jamaa anayeshangaa ni Dokta Gerald Ndika, kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo...
Mchoro unaoonyesha sehemu ya mbele ya jengo la utawala litakavyokua...
Mchoro unaonyesha jinsi moja ya madarasa yatakavyoonekana...

Wednesday, October 13, 2010

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS KIKWETE AMTEUA JAJI OTHMAN CHANDE KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA UENDESHAJI WA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA –LUSHOTO

-------------------------------------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhe. Jaji Othman Chande kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto (IJA). Mhe. Jaji Othman Chande ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Tanzania.

Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na ‘Schedule’ (1)(a) cha Sheria ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto, Sura ya 405.

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Mathias M. Chikawe (MB.), pia amewateua Wajumbe wengine 11 wa Baraza hilo. Mhe. Waziri amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto, Sura ya 405.

Uteuzi huu unafuatia kumalizika kwa muda uliowekwa kisheria wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Lushoto lililokuwa chini ya Uenyekiti wa Balozi Paul Rupia.

Uteuzi huu wa Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Uongozi la IJA-Lushoto umeanza tarehe 7 Agosti, mwaka huu (2010) na utakuwa wa baada ya miaka mitatu. Wajumbe wa Baraza la Chuo walioteuliwa ni:-

i. Mhe. Jaji Ernest Mwipopo (Mstaafu);

ii. Mhe. Jaji Aloysius K. Mujulizi, Mkuu wa Chuo – IJA ambaye atakuwa Katibu wa Baraza hilo;

iii. Prof. Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;

iv. Dkt. Eliuter G. Mushi, Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Mzumbe;

v. Bi. Mary S. Lyimo, kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

vi. Bi. Asina Omari, Wakili wa Kujitegemea na Mwanachama wa Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (Tanganyika Law Society);

vii. Bw. Francis Mutungi, Msajili wa Mahakama ya Rufani;

viii. Bi. Happiness P. Ndesamburo, Mkuu wa Kitengo cha mafunzo. Utafiti na Takwimu, Mahakama ya Tanzania;

ix. Bw. Mzee M. Mzee, Mhadhiri na Rais wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto;

x. Bw. Alex Benson, Mwakilishi wa Jumuiya ya Wafanyakazi IJA na;

xi. Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto;

Mhe. Rais pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria wanawatakia Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Bodi mafanikio katika utekelezaji wa wa majukumu yao mapya katika kukitumikia Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto.

Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto kilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge No. 3, mwaka 1998 na kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Agosti, 2001. Chuo hiki kinatoa mafunzo ya Stashahada (Diploma) na Cheti cha Sheria kwa Wanachuo wanaotarajia kuwa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Makarani katika wa Mahakama.

O.P.J. Mhaiki,

Katibu Mkuu,

Wizara ya Katiba na Sheria,

Makutano ya mtaa wa Mkwepu na Barabara ya Sokoine,

DAR ES SALAAM.

Thursday, October 7, 2010

OFISI YA MWANASHERIA MKUU SUMBAWANGA...

Wakili wa Serikali Mwandamizi Mfawidhi wa Kanda ya Songea Prudence Rweyongeza akiongea na wadau waliotembelea ofisini kwake hivi karibuni...
Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Kanda ya Sumbawanga...

Monday, October 4, 2010

MAHAKAMA MPYA YA MWANZO KILOLO

'Information panel' kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Kilolo, Iringa..
Sehemu ya majengo ya Mahakama ya Mwanzo Kilolo, Iringa yanayoendelea kujengwa...Inshallah, mwishoni mwa mwezi Oktoba kazi itakuwa imekamilika...
Kushoto ni 'parking' ya vyombo vya usafiri na kulia ni Kibanda cha Mlinzi...
Hii ni Kantini na chumba cha Mashahidi wakati wakisubiri kuitwa Mahakamani...

MAMBO YANABADILIKA...

Kulia ni Mheshimiwa Mary Moyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mafinga mkoani Iringa akiwa na wadau wa sheria katika kiwanja inapotarajiwa kujengwa Mahakama ya Mwanzo ya kisasa wilayani
Tunasonga mbele...Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Mbeya...jengo linaloonekana limefanyiwa ukarabati ili kuboresha mazingira ya kufanyia kazi...

Unaijua Shule ya Maadilisho Mbeya?

Jamaa kulia anaitwa Mwl. Leonard Isote akiwapa stori wadau waliotembelea Shule ya Maadilisho...iliyopo kilometa kama 40 kutoka Mbeya mjini...kushoto ni Ally Nampair, Injinia Mohamed Kitunzi na Dismas Chilala...Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Programu Maboresho ya Sekta ya Sheria imeiwezesha Shule kununua vifaa mbalimbali vikiwemo vitanda, magodoro n.k...
Mdau wa Katiba na Sheria Dismas Chilala nae katika photo la kumbukumbu na wanafunzi shuleni hapo...hapa ni bwenini...
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Maadilisho Mbeya a.k.a Mbeya Approved School wakipozi kwa photo la kumbukumbu...

Wednesday, September 29, 2010

WAKUU WA SASA ENZI HIZOOOO....

Unawajua hawa?...hawa ni wadau wakubwa sana katika sekta yetu ya sheria....hiii ni enzi hizoooooooo...

USO KWA USO NA RIDHIWANI KIKWETE MAKONGOLOSI - CHUNYA

Ni kweli Mbeya mbali kutoka Dar, lakini Chunya ni mbali zaidi. Makongolosi ni mbali zaidi...katika mishemishe za kiserikali ghafla jamaa huyu hapa...mshikaji kati hapo, Ridhiwani Kikwete, akiwa katika kazi za Chama katika Mjini Mdogo wa Makongolosi...hapa akisubiri kuzindua tawi la Wakereketwa...
Jamaa mkereketwa kushoto akisoma risala ya kumkaribisha 'mgeni mkuu'...
Wananchi wakishihudia kuzinduliwa kwa Tawi ...
Mshikaji akipiga kazi...

ZIARA YA MAKONGOLOSI - CHUNYA

Wadaub wakipata msosi katika 'best joint' pale Makongolosi...Chunya mkoani Mbeya. Unajua jina Makongolosi lilitokana na nini?...Jamaa walikuwa wanafnaya nini?...Ni kina nani?...Endelea...
Kulia jamaa ni Makamu Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Makongolosi, Chunya akielezea mipaka ya kiwanja ambacho inatajiwa kujengwa Mahakama ya Mwanzo Makangalosi. Kulia ni Injinia Mohamed Kitunzi kutoka Mahakama ya Tanzania, dar es Salaam akicheck. Mahakama hiyo pamoja na nyingine 19 zinatarajiwa kujengwa na Serikali kupitia Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria. Check chini Mahakama inayotumika sasa... Hapa ni Makongolosi, Chunya. Wadau wanasema Wazungu waliokuwa wakichimba dhahabu waliona hailipi, wakasema 'We're making loss...' Wabongo kwa kuchakachua wakasema 'Makongolosi'. Hili ni jengo la Mahakama ya Mwanzo Makongolosi lililojengwa kwa nguvu za wananchi then wakapigwa tafu na Serikali kama miongo miwili sasa...
Mhe. Sanga, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Makangalosi akiwapa stori wadau kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Mahakamani hapo...kulia Ally Nampair, then Injinia Mohamed Kitunzi kutoka Mahakama ya Rufaa na Dismas Chilala...
Mzee Malecela alifika Makongolosi pia...na kufungua Mahakama hiyo mwaka 1992. Enzi hizo akiwa 'Waziri Mkubwa' na Makamu wa Kwanza wa Rais...Big up Mzee!
Jaji Mwaikasu alifika Makongolosi pia...enzi hizo...na kuweka jiwe la Msingi la ujenzi ujenzi wa Mahakama hiyo...

CHANGAMOTO MAHAKAMA ZA MWANZO

Jengo la Mahakama ya Mwanzo Namanyere iliyopo Wilayani Nkasi, kilometa kama 85 kutoka Sumbawanga mjini. Jengo hilo pia tumika kama
Ndani ya Mahakama hiyo...
Kibanda ambacho mashahidi husubiria kuitwa Mahakamani ....
Maliwato ya Mahakama hiyo...