Wednesday, September 29, 2010

ZIARA YA MAKONGOLOSI - CHUNYA

Wadaub wakipata msosi katika 'best joint' pale Makongolosi...Chunya mkoani Mbeya. Unajua jina Makongolosi lilitokana na nini?...Jamaa walikuwa wanafnaya nini?...Ni kina nani?...Endelea...
Kulia jamaa ni Makamu Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Makongolosi, Chunya akielezea mipaka ya kiwanja ambacho inatajiwa kujengwa Mahakama ya Mwanzo Makangalosi. Kulia ni Injinia Mohamed Kitunzi kutoka Mahakama ya Tanzania, dar es Salaam akicheck. Mahakama hiyo pamoja na nyingine 19 zinatarajiwa kujengwa na Serikali kupitia Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria. Check chini Mahakama inayotumika sasa... Hapa ni Makongolosi, Chunya. Wadau wanasema Wazungu waliokuwa wakichimba dhahabu waliona hailipi, wakasema 'We're making loss...' Wabongo kwa kuchakachua wakasema 'Makongolosi'. Hili ni jengo la Mahakama ya Mwanzo Makongolosi lililojengwa kwa nguvu za wananchi then wakapigwa tafu na Serikali kama miongo miwili sasa...
Mhe. Sanga, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Makangalosi akiwapa stori wadau kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Mahakamani hapo...kulia Ally Nampair, then Injinia Mohamed Kitunzi kutoka Mahakama ya Rufaa na Dismas Chilala...
Mzee Malecela alifika Makongolosi pia...na kufungua Mahakama hiyo mwaka 1992. Enzi hizo akiwa 'Waziri Mkubwa' na Makamu wa Kwanza wa Rais...Big up Mzee!
Jaji Mwaikasu alifika Makongolosi pia...enzi hizo...na kuweka jiwe la Msingi la ujenzi ujenzi wa Mahakama hiyo...

1 comment:

  1. Kaka hapa umenikumbusha mbali sana, niliwahi kufika chunya, ni mbali utadhani unaenda nchi nyingine - kumbe ni Tanzania hapa hapa.

    Halafu ilikuwa gari ndogo sana, siyo 4x4. Lakini nili-enjoy sana.

    ReplyDelete