Wednesday, June 16, 2010

KISHERIASHERIA MWANZA

'Check' dira a.k.a Vision na Dhima a.k.a Mission ya Jamaa wa Katiba na Sheria
Katikati ni Mhe. Euphemia Mingi wa Mahakama ya Tanzania, kulia ni Mhe. Kisoka naye wa hukohuko wakipiga stori na Salum Mwalimu. 'Check' kipindi maalum leo saa 2:30 usiku Channel Ten!

'Mzee' Joe Mwakatobe wa RITA, jamaa wanaosajili, filisi na kudhamini wa pale Kipalapala Street, Upanga akilonga na Salum Mwalimu wa Channel Ten. Kwa mbali ni wadau wengine wa RITA.

Jamaa wa IJA - Institute of Judicial Administration akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la IJA katika maonesho ya Utumishi wa Umma pale Rock City.

Jamaa aliyekamata 'maiki' anaitwa Salum Mwalimu wa Channel Ten akipiga 'interview' na Mama Mtei wa Tume ya Utumishi wa Mahakama a.k.a Judicial Service Commission katika maonesho ya Utumishi wa Umma Mwanza jana.

Thursday, June 10, 2010

WAJUMBE WA BODI YA RITA

Wajumbe wa BODI ya Ushauri wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wakishuhudia uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Wakala huo.

RITA NA AHADI KWA MTEJA

Mambo ya Mkataba hayo...Mtaa wa Kipalapala, Muhimbili zilipo Ofisi za RITA.
Uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa RITA. Jamaa anaitwa Matth M. Chikawe, Waziri wa Katiba na Sheria, mdau wa Nachingwea na Mwakilishi wao, kushoto kwake anaitwa Vincent Mrisho, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (RITA) na Philip Saliboko, Kaimu Mtendaji Mkuu. Kulia ni Oliver P.J. Mhaiki, mwanaSongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Wednesday, June 9, 2010

MAMBO YA PORINI HAYO!

Mdau wangu wa karibu Jamal wa pale Maelezo kanitumia hii tupunguze mawazo kidogo!

Thursday, June 3, 2010

WADAU WA SHERIA KIKAZI MORO

Yanki vipi? Ushakumbuka Dubai ya uvuguvugu? Mshkaji anaitwa Geofrey Chami, Jamaa wa Mifumo ya Computer Katiba na Sheria eti anakula mada katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Morogoro. Yupo na wadau wengine wa Katiba na Sheria.
Unamjua huyu? Jamaa anaitwa Dkt. Frank Lekei wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akiwapiga shule wadau wa Katiba na Sheria katika mkutano wao wa Baraza la Wafanyakazi leo mjini Morogoro. hapa ni Oasis Hotel. Kulia kwake ni Hamis Mdee naye wa NHIF na Oliver Mhaiki Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria. Kwa mbaaali ni Rose Lugendo, Katibu Msaidizi wa Baraza.
Full ushirikiano: Mwenye suti black ni Mathias Chikawe, Waziri wa Katiba na Sheria, kushoto kwake Oliver Mhaiki, Katibu Mkuu na kulia kabisa Rose Lugendo, Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi wa Katiba na Sheria. Na kulee ni Simon Mhina wa TUGHE. Hii ni leo katika mkutano wa wafanyakazi Morogoro. Hapa walikuwa wakiimba 'Solidarity Forever....'
Jamaa anaitwa Mathias M. Chikawe a.k.a Matth, mdau wa kusini a.k.a Mwakilishi wa WanaNachingwea Mjengoni na Waziri wa Katiba na Sheria. Hapa alikuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi, Hoteli ya Oasis Mji kasoro bahari - Morogoro. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Oliver Mhaiki, mwana Songea Mjini na jamaa anayecheck ni Simon Msuya, jamaa wa TUGHE. Hii leo!