Thursday, June 3, 2010

WADAU WA SHERIA KIKAZI MORO

Yanki vipi? Ushakumbuka Dubai ya uvuguvugu? Mshkaji anaitwa Geofrey Chami, Jamaa wa Mifumo ya Computer Katiba na Sheria eti anakula mada katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Morogoro. Yupo na wadau wengine wa Katiba na Sheria.
Unamjua huyu? Jamaa anaitwa Dkt. Frank Lekei wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akiwapiga shule wadau wa Katiba na Sheria katika mkutano wao wa Baraza la Wafanyakazi leo mjini Morogoro. hapa ni Oasis Hotel. Kulia kwake ni Hamis Mdee naye wa NHIF na Oliver Mhaiki Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria. Kwa mbaaali ni Rose Lugendo, Katibu Msaidizi wa Baraza.
Full ushirikiano: Mwenye suti black ni Mathias Chikawe, Waziri wa Katiba na Sheria, kushoto kwake Oliver Mhaiki, Katibu Mkuu na kulia kabisa Rose Lugendo, Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi wa Katiba na Sheria. Na kulee ni Simon Mhina wa TUGHE. Hii ni leo katika mkutano wa wafanyakazi Morogoro. Hapa walikuwa wakiimba 'Solidarity Forever....'
Jamaa anaitwa Mathias M. Chikawe a.k.a Matth, mdau wa kusini a.k.a Mwakilishi wa WanaNachingwea Mjengoni na Waziri wa Katiba na Sheria. Hapa alikuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi, Hoteli ya Oasis Mji kasoro bahari - Morogoro. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Oliver Mhaiki, mwana Songea Mjini na jamaa anayecheck ni Simon Msuya, jamaa wa TUGHE. Hii leo!

No comments:

Post a Comment