Wednesday, September 29, 2010
USO KWA USO NA RIDHIWANI KIKWETE MAKONGOLOSI - CHUNYA
ZIARA YA MAKONGOLOSI - CHUNYA
Wadaub wakipata msosi katika 'best joint' pale Makongolosi...Chunya mkoani Mbeya. Unajua jina Makongolosi lilitokana na nini?...Jamaa walikuwa wanafnaya nini?...Ni kina nani?...Endelea...
Kulia jamaa ni Makamu Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Makongolosi, Chunya akielezea mipaka ya kiwanja ambacho inatajiwa kujengwa Mahakama ya Mwanzo Makangalosi. Kulia ni Injinia Mohamed Kitunzi kutoka Mahakama ya Tanzania, dar es Salaam akicheck. Mahakama hiyo pamoja na nyingine 19 zinatarajiwa kujengwa na Serikali kupitia Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria. Check chini Mahakama inayotumika sasa... Hapa ni Makongolosi, Chunya. Wadau wanasema Wazungu waliokuwa wakichimba dhahabu waliona hailipi, wakasema 'We're making loss...' Wabongo kwa kuchakachua wakasema 'Makongolosi'. Hili ni jengo la Mahakama ya Mwanzo Makongolosi lililojengwa kwa nguvu za wananchi then wakapigwa tafu na Serikali kama miongo miwili sasa...
Mhe. Sanga, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Makangalosi akiwapa stori wadau kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Mahakamani hapo...kulia Ally Nampair, then Injinia Mohamed Kitunzi kutoka Mahakama ya Rufaa na Dismas Chilala...
Mzee Malecela alifika Makongolosi pia...na kufungua Mahakama hiyo mwaka 1992. Enzi hizo akiwa 'Waziri Mkubwa' na Makamu wa Kwanza wa Rais...Big up Mzee!
Tuesday, September 21, 2010
MAHAKAMA YA MWANZO YA KISASA LUGOBA - CHALINZE
Unalifahamu eneo hili?...kilomita kama 15 kutoka Chalinze kuelekea Segera, upande wa kulia majengo haya yanaonekana. Ni Majengo mapya ya kisasa ya Mahakama ya Mwanzo Msoga-Lugoba...mita chini ya 100 kutoka barabara kuu... kumbe tunaweza kujenga ... kazi iendelee...kwa kazi zaidi
Ndani...kwa pilato...
Vijana wa Katiba na Sheria, kutoka shoto Tumsifu Kimaro, Andrea Eriyo, Ally Nampair na Dismas Chilala wakiwa Mahakamani hapo...
Nyumba ya vyumba vitatu yenye umeme na maji kwa ajili ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Lugoba. Nyumba hii ipo ndani ya eneo la Mahakama hiyo ya kisasa...
Maliwatoni Mahakamani hapo, tena na maji ya bomba...
Jengo la Mahakama hiyo kwa nje...umeona viyoyozi hivyo?
Jengo lenye paa nyekundu ndio Mahakama yenyewe, kulia ni kantini na chumba cha mashahidi wakati wanasubiri kuitwa Mahakamani na kushoto ni kibanda cha mlinzi...
Mahakamani ndani...
Nyumba ya vyumba vitatu yenye umeme na maji kwa ajili ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Lugoba. Nyumba hii ipo ndani ya eneo la Mahakama hiyo ya kisasa...
Maliwatoni Mahakamani hapo, tena na maji ya bomba...
Jengo la Mahakama hiyo kwa nje...umeona viyoyozi hivyo?
Jengo lenye paa nyekundu ndio Mahakama yenyewe, kulia ni kantini na chumba cha mashahidi wakati wanasubiri kuitwa Mahakamani na kushoto ni kibanda cha mlinzi...
Mahakamani ndani...
Monday, September 20, 2010
JESHI LA POLISI LAPEWA ZANA ZA KAZI
Benas Mayogu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akimkabidhi Afande Peter Kivuyo, Naibu Kamishna wa Polisi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai baadhi ya vifaa vya upelelezi vilivyonunuliwa kupitia Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria (LSRP) inayoratibiwa na Wizara ya Katiba na Sheria. Vifaa hivyo ni Kamera, Computers, Printers na vina thamani ya zaidi ya Shs 104 milioni. Baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa.
Wanafunzi, Walimu 'Law School' baada ya kazi nzito!
Walimu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania a.k.a Law School of Tanzania kutoka Tanzania wakiwa na wenzao kutoka Uingireza chini ya International Law Project (ILP) katika picha ya kumbukumbu pale Yombo UDSM mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga walimu kutoka UK waliokuwepo Bongo kwa wiki mbili wakiwapiga shule wanafunzi wa Law School. ILP inaisaidia Law School kutoa mafunzo ya vitendo na kujenga uwezo wa walimu wa Law School katika kutoa mafunzo hayo. Endelea...
Wakili in the making...jamaa aliyekamata 'mike' anaitwa Salvatory Stemius, mwanafunzi akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo mbele ya wanafunzi na wakufunzi...kushoto kwake ni Dkt. Gerald Ndika a.k.a Uncle G, Kaimu Mkuu wa Law School.
Picha ya ukumbusho...wanafunzi na walimu nje ya Yombo, UDSM.
Jamaa kushoto anaitwa Icah Peart, Wakili wa Kujitegemea kuanzia miaka ya 1970 kule Uingereza...hadhi yake sasa ni QC a.k.a Queen's Counsel...wanasheria mnajiua hiyo maana yake nini. Kulia ni Dkt. Gerald Ndika, Kaimu Mkuu wa 'Law School' akimkabidhi zawadi baada ya kuwapiga shule vijana wake kwa wiki mbili pale Mlimani ambapo mafunzo hayo yanaendeshwa kwa muda.
Subscribe to:
Posts (Atom)