Walimu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania a.k.a Law School of Tanzania kutoka Tanzania wakiwa na wenzao kutoka Uingireza chini ya International Law Project (ILP) katika picha ya kumbukumbu pale Yombo UDSM mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga walimu kutoka UK waliokuwepo Bongo kwa wiki mbili wakiwapiga shule wanafunzi wa Law School. ILP inaisaidia Law School kutoa mafunzo ya vitendo na kujenga uwezo wa walimu wa Law School katika kutoa mafunzo hayo. Endelea...
Wakili in the making...jamaa aliyekamata 'mike' anaitwa Salvatory Stemius, mwanafunzi akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo mbele ya wanafunzi na wakufunzi...kushoto kwake ni Dkt. Gerald Ndika a.k.a Uncle G, Kaimu Mkuu wa Law School.
Picha ya ukumbusho...wanafunzi na walimu nje ya Yombo, UDSM.
Jamaa kushoto anaitwa Icah Peart, Wakili wa Kujitegemea kuanzia miaka ya 1970 kule Uingereza...hadhi yake sasa ni QC a.k.a Queen's Counsel...wanasheria mnajiua hiyo maana yake nini. Kulia ni Dkt. Gerald Ndika, Kaimu Mkuu wa 'Law School' akimkabidhi zawadi baada ya kuwapiga shule vijana wake kwa wiki mbili pale Mlimani ambapo mafunzo hayo yanaendeshwa kwa muda.
No comments:
Post a Comment